English
Français

Kozi ya Uchongaji

Uchongaji wa madini ya vito kutoka Lapidary Training Centre - Dar-es-Salaam.

Ndani ya wiki 10 utajifunza mbinu mbalimbali za uchongaji na ung'arishaji wa madini ya vito. Tofauti na kozi ya wiki 2 ni kwamba utapata muda mrefu wa kufanya mazoezi ya ukataji. Mashine na vifaa vya kisasa vipo kwa ajili yako. Tunafundishia mashine za Ultra-Tec V5D, mashine mbalimbali za cabbochon, misumeno, pamoja na vifaa vya kuchongea maumbo tofautitofauti.

Utangulizi wa jiologia, kugredi, kutathimini, na kupima madini kabla na baada ya kuyachonga ni sehemu ya mafuzo. Utaweza kuchonga madini mbalimbali kwa maumbo tofautitofauti na saizi mbalimbali. Utaanza kwa kutengeneza umbo la duara na baadae kuendelea na maumbo mengine ya kisasa. Maumbo kama vile mraba, pembe tatu, mstatili, umbo la yai, moyo na mengine mengi ni sehemu ya mazoezi utakayofanya.

Mwalimu mwenye uzoefu wa kutosha atakuelekeza na kukufundisha jinsi ya kukata na kupata kito chenye kung'aa na kupendeza. Maelezo muhimu ya usalama kuhusu utumiaji wa mashine na vifaa vinginevyo yatatolewa kwa ufasaha wakati wa vipindi. Cheti kitatolewa kwa kila mwanafunzi atakaye hitimu na kufanya vizuri darasani.

Baadhi ya vito vitatolewa kwa ajili ya mazoezi.

  • garnet
  • citrine
  • amethyst
  • aquamarine
  • scapolite
  • zircon
  • rock crystal
  • ruby zoisite
  • corundum (ruby and sapphire)
  • tourmaline
  • amazonite
  • iolite
  • sunstone
  • moonstone
  • opal
  • kyanite, etc...

Lakini pia unaweza kuleta vito vyako unavyovipendelea. Vile vile mwisho wa kozi utakabidhiwa vito vyote utakavyokuwa umevitengeneza.

Baada ya wiki 10 za masomo utaweza kuendelea na mazoezi na kukata vito kwa wateja wako wa kwanza. Mwalimu atakuwepo na kukuelekeza pale utakapokuwa na swali lolote.


Masomo yataanza saa 3.00 asubuhi hadi 11.00 jioni. Mapumziko kwa ajili ya chakula cha mchana ni muda wa saa moja. Kila mwanafunzi atajitegemea kwa usafiri na chakula cha mchana. Lakini chakula kitaweza kuandaliwa.
Ada kwa wiki 10 ni US$ 1'250.-

Usaji wa Kozi ya Uchongaji mawe



Vito vilivyokatwa na wanafunzi









































Have a look into the class room with a faceting class under way 2019.




Ni furaha ya namna gani kumwanzishia mwanafunzi dhana na kuona jinsi akuavyo na kupata mwelekeo na uvumbuzi mpya.



Kozi
Vifaa
Matukio yajayo
Madini & migodi
Kazi zangu
Sifa zangu
Mawasiliano
Mwanzo   Notisi ya faragha
logo

© Hati miliki ya picha zote Noreen Masaki