English

Kozi ya jemolojia

Utambuzi wa madini ya vito katika Lapidary Training Centre - Dar es Salaam.

Kipindi cha wiki moja utajifunza jinsi ya kupima, kutambua na kutofautisha aina mbalimbali za madini.

Kozi hii imebuniwa ili kukupa utangulizi wa kinadharia na vitendo kwenye fani ya jemolojia. Ili upate ujuzi wa kuchunguza na kutambua kwa usahihi madini ya vito, yanayopatikana ardhini na yale ya kutengenezwa kiwandani.

Kwa faida ya uchache wa wanafunzi darasani na maelekezo binafsi, wanafunzi hupata na kuendeleza kwa haraka ujuzi wenye thamani kubwa katika sekta hii ya madini. Itakugharimu wiki moja tu kupata ujuzi na kutambulika kikamilifu kama mtaalamu aliyehitimu mafunzo.

Mara kwa mara wanafunzi wamekuwa wakiunda na kuendeleza uhusiano wa kibiashara walioujenga kipindi cha masomo na kuwa wenye mafanikio. Hakuna pengine isipokuwa Lapidary Training Centre kwa kujenga mahusiano na kutafuta mshiriki bora katika biashara yako. Cheti kutoka Lapidary Training Centre ni alama ya uadilifu na utaalamu wako na funguo za mafanikio ya kazi yako.

Mtaala

  • Almasi na vigezo vyake
  • Aina mbalimbali za madini ya vito na uotaji wake
  • Utambuzi wa madini ya vito kwa kutumia muonekano na sifa zake
  • Utumiaji na umiliki fasaha wa vifaa vya jemoloji
  • Tafsiri sahihi ya majibu yanayosomeka kwenye vyombo vya jemoloji
  • Imitations na vito feki
  • Vito vya rangi na vigezo vyake
  • Ukataji na uongezaji thamani wa madini ya vito
  • Masoko


Masomo yataanza saa 3.00 asubuhi hadi saa 10.00 alasiri, mapumziko ya chakula cha mchana ni muda wa saa moja.
Ada kwa wiki moja ni US$ 300.-

Usaili wa kozi ya jemolojia



Wanafunzi wa somo la jemolojia
















Ni furaha ya namna gani kumwanzishia mwanafunzi dhana na kuona jinsi akuavyo na kupata mwelekeo na uvumbuzi mpya.



Kozi
Vifaa
Matukio yajayo
Madini & migodi
Kazi zangu
Sifa zangu
Mawasiliano
Mwanzo   Notisi ya faragha
logo

© Hati miliki ya picha zote Noreen Masaki