English

Kabla na baada ya kurudia kukata

Nimetoa vipaumbele kwenye, uzuri kwanza, ikafuata ukubwa
na mwisho kuzingatia uzito.

Vifuatavyo ni vito vya thamani vilivyorudiwa tukatwa, kwa sababu uzuri wake uliharibiwa kwa kutokuzingatia vipimo sahihi. Inawezekana vilikatwa kwa kuzingatia uzito tu, au mashine iliyotumika ilikuwa ya zamani sana, au mashine isiyowezesha kusoma pembe sahihi, au mkataji hakuwa na uzoefu, au ni jumla ya vyote hivyo.

Jionee mwenyewe tofauti kubwa baada ya kurudia kukata. Ndipo sasa uzuri na asili ya kweli ya kito yaweza kuonekana.
Kabla Baada
Vipimo : 10.00 x 7.90 mm
Uzito : 2.90 ct
Umbo na faseti zisizolingana,
kusababisha kupungua kwa uzuri.
Vipimo : 9.27 x 7.28 x 5.79 mm
Uzito : 1.60 ct
Kukata kwa kuzingatia uzuri.
Uzito uliopotea -44.82%
 

 

Vipimo : 9.36 x 7.88 x 4.78 mm
Uzito : 2.91 ct
Umbo lisilolingana na uwazi katikati ya kito,
kusababisha kupungua kwa uzuri.
Vipimo : 7.99 x 6.77 x 4.59 mm
Uzito: 1.64 ct
Kukata kwa kuzingatia uzuri.
 

 

Vipimo : 16.23 x 14.01 mm
Uzito : 12.89 ct
Umbo lisilolingana na uwazi katikati ya kito,
kusababisha kupungua kwa uzuri.
Vipimo : 15.50 x 11.68 mm
Uzito : 8.95 ct
Kukata kwa kuzingatia uzuri.
Uzito uliopotea -30.56%
 

 

Vipimo : havijabadilika
Uzito : 3.17 ct
Emerald ikionyesha kuakisi giza na
uchafu kuakisiwa mara kadhaa.
Vipimo : havijabadilika
Uzito: 3.01 ct
Emerald hii imerudiwa kukatwa kidogo sana, ili kuondoa sehemu kubwa iliyokuwa na uchafu, na kuboresha faseti zilizokuwa na giza.
Umuhimu ulikuwa kwenye kuzingatia uzito. Uzito uliopotea -5.04%
 

 

Vipimo :
Uzito : 5.26 ct
Tanzanite yenye uwazi katikati,
kusababisha kupungua kwa uzuri.
Vipimo : 11.56 x 7.88 x 5.71 mm
Uzito : 3.36 ct
Kukata kwa kuzingatia uzuri.
Uzito uliopotea -36.12%
 

 

Vipimo : 12.40 x 12.40 x 5.30 mm
Uzito : 5.99 ct
Umbo lisilolingana na uwazi katikati ya kito,
kusababisha kupungua kwa uzuri.
Mhimili-C umesababisha giza kwenye Tourmaline.
Vipimo : 10.46 x 7.52 x 4.76 mm
Uzito : 3.03 ct
Kuondolewa kwa giza lililokuwa likiakisiwa na mhimili-C.
Kukata kwa kuzingatia uzuri.
Uzito uliopotea -49.41%
 

 

 

 

V5D with digital angle dialVito vyote hapo juu vimerudiwa kukatwa kwa kutumia mashine ya digitali ya Ultra-Tec V5D.

 

Noreen Masaki May 2018Kozi
Vifaa
Matukio yajayo
Madini & migodi
Kazi zangu
Sifa zangu
Mawasiliano
Mwanzo   Notisi ya faragha
logo

Hati miliki ya picha zote Noreen Masaki