English

Kozi ya Uchongaji

Uchongaji wa madini ya vito kutoka Lapidary Training Centre - Dar-es-Salaam.

Ndani ya wiki mbili au wiki nne utajifunza mbinu mbalimbali za uchongaji na ung'arishaji wa madini ya vito. Mashine na vifaa vya kisasa vipo kwa ajili yako. Tunafundishia mashine za Ultra-Tec, mashine mbalimbali za cabbochon, misumeno, pamoja na vifaa vya kuchongea maumbo tofautitofauti. Kugredi, kutathimini, na kupima madini kabla na baada ya kuyachonga ni sehemu ya mafunzo. Utaweza kuchonga madini mbalimbali kwa maumbo tofautitofauti na saizi mbalimbali. Utaanza kwa kutengeneza umbo la duara na baadae kuendelea na maumbo mengine ya kisasa.

Mwalimu mwenye uzoefu wa kutosha atakuelekeza na kukufundisha jinsi ya kukata na kupata kito chenye kung'aa na kupendeza. Maelezo muhimu kuhusu utumiaji wa mashine na vifaa vinginevyo yatatolewa kwa ufasaha wakati wa vipindi. Cheti kitatolewa kwa kila mwanafunzi atakaye hitimu na kufanya vizuri darasani.

Baadhi ya vito vitatolewa kwa ajili ya mazoezi, lakini pia unaweza kuleta vito unavyovipendelea. Vile vile mwisho wa kozi utakabidhiwa vito vyote utakavyokuwa umevitengeneza.

Baada ya wiki mbili za masomo utaweza kuendelea na mazoezi ili upate uzoefu wa kutosheleza wa kozi uliyohitimu. Mwalimu atakuwepo na kukuelekeza pale utakapokuwa na swali lolote.


Masomo yataanza saa 3.00 asubuhi hadi 11.00 jioni. Mapumziko kwa ajili ya chakula cha mchana ni muda wa saa moja.
Kila mwanafunzi atajitegemea kwa usafiri na chakula cha mchana.
Ada kwa wiki mbili ni US$ 500.-
Ada kwa wiki nne ni US$ 870.-

Usaji wa Kozi ya Uchongaji mawe



Vito vilivyokatwa na wanafunzi wangu

Citrine by Paul A. Makunda
some other stones I have cut

Rock crystal by John B.
Testimonial

Garnet by Catherine V.

Rock crystal

Amethyst-Citrin by Goodluck C.

Garnet by Goodluck C.

Topaz by Kohkazu

Scapolite by Kohkazu

Aquamarin by Kohkazu

Scapolite by Percy

Amethyst by Raymond Mulder
more stones I cut during class

Gems cut by Kamran Avin

Citrine by Sethi

Rock crystal by Reginald

Citrine by Reginald


Wanafunzi wa kozi ya uchongaji wa madini ya vito




































Ni furaha ya namna gani kumwanzishia mwanafunzi dhana na kuona jinsi akuavyo na kupata mwelekeo na uvumbuzi mpya.



Kozi
Vifaa
Matukio yajayo
Madini & migodi
Kazi zangu
Sifa zangu
Mawasiliano
Mwanzo   Notisi ya faragha
logo

© Hati miliki ya picha zote Noreen Masaki