English

Kozi fupi ya Uchongaji wa Madini ya Vito

Uchongaji wa madini ya vito - Lapidary Training Centre - Dar es Salaam.

Kozi hii imeandaliwa ili kutimiza ombi maalumu kutoka kwa wateja wetu. Kama huna muda wa kutosha, au una mashine zako, basi kozi hii ndiyo sahihi kwako.

- Yaliyomo katika darasa hili ni sawa sawa na ya darasa la wiki mbili. -

Ndani ya siku tano (5) utajifunza mbinu mbalimbali za uchongaji na ung'arishaji wa madini ya vito. Mashine na vifaa vya kisasa vipo kwa ajili yako. Tunafundishia mashine za Ultra-Tec, mashine mbalimbali za cabbochon, misumeno, pamoja na vifaa vya kuchongea maumbo tofautitofauti. Kugredi, kutathimini, na kupima madini kabla na baada ya kuyachonga ni sehemu ya mafunzo. Utaweza kuchonga madini mbalimbali kwa maumbo tofautitofauti na saizi mbalimbali. Utaanza kwa kutengeneza umbo la duara na baadae kuendelea na maumbo mengine ya kisasa.

Mwalimu mwenye uzoefu wa kutosha atakuelekeza na kukufundisha jinsi ya kukata na kupata kito chenye kung'aa na kupendeza. Maelezo muhimu kuhusu utumiaji wa mashine na vifaa vinginevyo yatatolewa kwa ufasaha wakati wa vipindi. Cheti kitatolewa kwa kila mwanafunzi atakaye hitimu na kufanya vizuri darasani.

Baadhi ya vito vitatolewa kwa ajili ya mazoezi, lakini pia unaweza kuleta vito unavyovipendelea. Vile vile mwisho wa kozi utakabidhiwa vito vyote utakavyokuwa umevitengeneza.


Masomo yataanza saa 3.00 asubuhi hadi 11.00 jioni. Mapumziko kwa ajili ya chakula cha mchana ni muda wa saa moja. Ada kwa wiki hii moja ni US$ 300.- Kila mwanafunzi atajitegemea kwa usafiri na chakula cha mchana.

Usajili wa Kozi fupi ya Uchongaji wa mawe



Wanafunzi waliohitimu mafunzo ya uchongaji wa madini ya vito





Testimonials
by Harold Lindsay,                Canada 2016
by John Bosco Gatsimbanyi, Uganda 2014




Ni furaha ya namna gani kumwanzishia mwanafunzi dhana na kuona jinsi akuavyo na kupata mwelekeo na uvumbuzi mpya.



Kozi
Vifaa
Matukio yajayo
Madini & migodi
Kazi zangu
Sifa zangu
Mawasiliano
Mwanzo   Notisi ya faragha
logo

© Hati miliki ya picha zote Noreen Masaki